Kesi ya mauaji ya Kanumba yamsubiri Lulu mwakani |
KESI ya kuua bila kukusudia inayomkabili mtoto mzuri wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ imewekwa kiporo kufuatia kuwepo kwa kesi nyingi za mauaji mahakamani na uhaba wa majaji kwani wengi wataenda likizo.
Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake, Steven Kanumba, Aprili 7, 2012 maeneo ya Vatican-Sinza jijini Dar.Kifo cha Kanumba kilichotokea nyumbani kwake, kilidaiwa kilitokana na kuangukia sehemu ya nyuma ya kichwa ambapo alipata mtikisiko wa ubongo kisha kuzikwa kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar.
CREDITS: GPL
0 Response to "MASKINI LULU!! JINAMIZI LA MAUAJI KUMFUNGULIA MWAKA MPYA WA 2015!!!! YADAIWA MAUAJI YAMEZIDI!!!!"
Post a Comment