ZA UKWELI SANA

TANZANIA KUWEKA HISTORIA DUNIANI!!! SABABU 5 ZA HAPPINESS KUTAWAZWA MALKIA WA DUANIA!!!!

Happiness Watimanywa katika mapozi

Mshindi wa Shindano la Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa, Jumamosi ya wiki iliyopita, alikwea pipa kuelekea jijini London, Uingereza kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss World, yanayotarajiwa kutimua vumbi Desemba 14, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Excel London.

Licha ya ‘magumashi’ ya Kamati ya Miss Tanzania, kwa kumpa maandalizi duni, Happiness atashinda kwa vigezo vifuatavyo:

1. Mvuto wa Sura. Happiness ana sura ambayo ikipambwa na tabasamu kila jaji ataweka tick!
2. Tumbo lisiloshiba. baba!! Masaa 24 tumbo la Happy halitoi mistari ya kontua. Umbo lake halijaathiriwa na chips mayai!

3. Uwezo wa kujieleza kwa ufasaha. Happiness hapapatiki anaposogezewa 'microphone' na hana 'eeeh... eeeh' anapojibu swali.
4. Elimu: Kiwango cha Elimu kinampa uwezo wa kupambana kimataifa.
5. Nchi. Kumekuwa na ongezeko la 'presha' kwamba Miss World isipendelee nchi zilizoendelea pekee. Tanzania kama nchi inayopambana kutambulika kimataifa inawezekana ikapewa jicho tofauti!

KUMBUKA MUNGU ALICHAGUA VITU DHAIFU KUFANYA MAKUBWA!!!! SEMA AMINA!!!

0 Response to "TANZANIA KUWEKA HISTORIA DUNIANI!!! SABABU 5 ZA HAPPINESS KUTAWAZWA MALKIA WA DUANIA!!!!"

Post a Comment