ZA UKWELI SANA

NI KAMA JARIBU!! VIELELEZO KUTOKA RITA KASHFA YA KUGHUSHI YA SITTI MTEMVU VYATUA KWA KAMANDA KOVA!!!!!

Vielelezo vya Sitti toka RITA vyatua Polisi



Dar es Salaam/ Arusha. Kashfa ya aliyekuwa Miss Tanzania, Sitti Mtemvu imechukua sura mpya baada ya Wakala wa Uzazi, Vifo na Ufilisi (Rita) kusema kuwa wamekamilisha upekuzi wa taarifa alizotumia kuombea cheti cha kuzaliwa na vielelezo hivyo vimelekwa polisi vikafanyiwe kazi.

Wakizungumza na gazeti la Mwananchi kwa nyakati tofauti jana, Ofisa mtendaji mkuu wa Rita, Phillip Saliboko na Meneja masoko na mawasiliano, Josephat Kimaro walisema upekuzi wa nyaraka zilizotumiwa na Sitti uliofanywa na wanasheria wao, tayari umekamilika.


Sitti Mtemvu aliingia kwenye kashfa ya kudanganya umri wake na nyaraka zake mbalimbali zilionyesha alizaliwa 1989, umri ambao umepitiliza ule unaotakiwa kwa mshiriki wa mashindano ya Miss Tanzania, huku cheti chake kikionyesha alizaliwa 1991, hivyo kulazimika kuvua taji hilo.

0 Response to "NI KAMA JARIBU!! VIELELEZO KUTOKA RITA KASHFA YA KUGHUSHI YA SITTI MTEMVU VYATUA KWA KAMANDA KOVA!!!!!"

Post a Comment